Ijumaa 7 Novemba 2025 - 10:38
Je, damu inayobakia kwa mnyama baada ya kuchinjwa ni najisi?

Hawza/ Ayatullah Ali Khamenei amejibu istiftaa kuhusiana na hukmu ya damu inayobakia kwa mnyama baada ya kuchinjwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika masuala ya fiqhi na hukmu za kisheria, kujua hukmu sahihi kuhusiana na damu inayobakia kwa mnyama aliyechinjwa ni jambo lenye umuhimu maalumu, kwani suala hili linahusiana moja kwa moja na tohara na najisi ya nyama pamoja na bidhaa nyingine zinazotokana na wanyama. Waumini wengi na wale wanaofanya kazi katika sekta za kuchinja wanyama huhitaji kufahamu hukmu hii ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kidini ipasavyo:

Swali:
Je, damu inayobakia kwenye mwili wa mnyama baada ya kuchinjwa na hutoka taratibu, ni najisi?

Jawabu:
Ikiwa baada ya kuchinjwa damu itatoka kwa hali ya kawaida na kwa ukamilifu, na sehemu ya kuchinjia pamoja na damu iliyomwagika zikasafishwa, basi damu inayobakia ndani ya mwili wa mnyama na ile itakayofuata kutoka baada ya hapo, ni tohara (safi, si najisi).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha